01. Tuhuma za ad-Duwaysh dhidi ya al-Albaaniy


Kuna ndugu katika dini amenionyesha yale yaliyoandikwa na Dr Muusa ad-Duwaysh akimraddi mwandishi wa gazeti la ”as-Salafiyyah”. Kijitabu chake kinaitwa ”Min-at-Takfiyr ilaat-Tafjiyr” na ndani yake mna matusi, kumdhulumu na kumzulia uongo al-Albaaniy (Rahimahu Allaah). Kwa ajili hiyo nikaona nina kila haki ya kumtetea al-Albaaniy (Rahimahu Allaah).

Kijana huyu aliyeghurika amemtukana Shaykh al-Albaaniy ikiwa ni pamoja vilevile na matusi yafuatayo:

1- Alikuwa Takfiyriy.

2- Alikuwa na tamaa za siasa.

3- Alikuwa akimfuata kibubusa Sayyid Qutwub.

Amemfananisha vilevile na Hasan at-Twuraabiy, Zayniy Dahlaan na makhurafi wengine.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 22/01/2018