01. Sababu ya kutunga kitabu “Kitaab-ul-I´tiqaad”

Siku ya ijumaa tarehe 13 Shawwaal mwaka wa 573 alinikhabarisha muheshimiwa Shaykh Abu Sa´iyd ´Abdul-Jabbaar bin Yahyaa bin ´Aliy bin Hilaal al-A´rabiy kwa njia ya kunisomea na mimi nasikiliza. Amesema: Muheshimiwa Abul-Husayn Muhammad bin Muhammad bin al-Farraa´ amsema:

Himdi zote anastahiki Allaah mpaka aridhie. Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, Aliyetukuka, Aliye juu kabisa. Himdi zote ni za Allaah ambaye anastahiki kushukuriwa pasi na kikomo. Himdi zote anastahiki Allaah ambaye ametuumba baada ya kutokuwepo, akatujaalia kuwa katika Ummah bora na akatuteulia kiumbe Chake bora na Mtume Wake mtukufu zaidi kutuongoza. Amemfanya kuwa mtu wa kwanza aliyetangulia inapokuja katika manzilah na Mtume bora kabisa inapokuja katika ujumbe –Allaah amsifu na familia yake wazuri swalah ambayo itawakusanya wote pamoja.

Allaah atukinge sisi na nyinyi juu ya kujikafilisha mambo tusiyoyaweza wala kudai tusiyoyamairi. Allaah atulinde sisi na nyinyi kutokamana na Bid´ah na uongo ambavyo ndio uovu na uchafu mkubwa zaidi ambavyo mtu anaweza kuwa navyo.

Hakika umeniuliza kuhusu ´Aqiydah yangu na yale ninayomwabudu Mola wangu (´Azza wa Jall) ili uweze kuyafuata na matokeo yake ufuzu kutokamana na Bid´ah na matamanio yenye kupotosha na utunukiwe na Allaah (´Azza wa Jall) ngazi za juu. Hivyo nakujibu yale uliyoniuliza hali ya kutaraji thawabu kubwa kutoka kwa Allaah na kuogopa adhabu Yake kali na namtegemea juu ya kuzungumza maneno yaliyo ya sawa.

  • Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 20/02/2019