Hakika utafiti wetu wa Qur-aan, Sunnah na mapokezi ya Salaf katika suala hili muhimu imetubainikia ya kwamba mwanamke anapotoka nyumbani kwake, basi ni wajibu kwake kuufunika mwili wake wote isipokuwa uso na mikono yake (ikiwa atataka kufanya hivo) pamoja na kwamba asionyeshe kitu katika mapambo yake pasi na kujali ni vazi lepi alilovaa. Jilbaab yake inatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:

1 – Ni wajibu kwake kufunika mwili wake wote isipokuwa yale yaliyovuliwa.

2 – Yenyewe kama yenyewe isiwe ya mapambo.

3 – Isiwe yenye kuonyesha kwa ndani.

4 – Iwe pana na yenye kupwaya.

5 – Isiwe ni yenye kutiwa manukato.

6 – Isiwe ni yenye kufanana na vazi la wanaume.

7 – Isiwe ni yenye kufanana na vazi la wanawake wa kikafiri.

8 – Isiwe ni vazi lenye kufanya watu kukataka kumtazama na kutambulika.

Itambulike kuwa baadhi ya masharti haya sio maalum kwa wanawake peke yao; yanawahusu wanaume na wanawake wote wawili. Kama ambavyo baadhi ya masharti hayo ni haramu kwake moja kwa moja, sawa awe nyumbani kwake au nje. Kama mfano wa hayo masharti matatu ya mwisho. Lakini kwa vile maudhui yangu mimi inahusu vazi lake la jilbaab pale anapotoka, basi ntakomekea hapo. Kwa hivo nitafafanua yale niliyoyataja kwa jumla na kutaja dalili juu ya yale niliyoyataja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 07/11/2017