Hakika Allaah pekee ndiye anayejua ni namna gani maasi yalivyo na athari mbaya na yanavyodhuru moyoni na mwilini hapa duniani na Aakhirah.

Moja katika athari zake ni kwamba yanazuia elimu. Hakika ya elimu ni nuru ambayo Allaah anaiweka ndani ya moyo. Maasi yanaizima nuru hiyo. Pindi Imaam ash-Shaafi´iy alipoketi mbele ya Maalik na akaanza kumsomea, basi Maalik alipendekezwa namna zilivyokuwa  akili, busara na ukamilifu wa uelewa wake. Hapo ndipo akamwambia:

”Naona kuwa Allaah ameiweka nuru kwenye moyo wako. Usiizime kwa giza la maasi.”

ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Nilimshtakia Wakiy´ juu ya kuzoroto kwa kumbukumbu yangu. Akaninasihi kuacha maasi na kusema: “Tambua kuwa elimu ni fadhla na hampi mtenda madhambi.”

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 65
  • Imechapishwa: 28/12/2017