1- Ibn-ul-Mundhir (kfrk. 318) tabaka 11

adh-Dhahabiy ameelezea wasifu wake katika ”Tadhkirat-ul-Huffaadhw” na akasema:

”Haafidhw wa kipekee, ´Allaamah na Faqiyh Abu Bakr Muhammad bin Ibraahiym bin al-Mundhir an-Naysaabuuriy. Alikuwa ni Shaykh wa Haram na mwandishi wa vitabu visivokuwa na mfano kukiwemo:

1 – al-Mabsuutw fiyl-Fiqh

2 – al-Ishraaf fiy Ikhtilaaf-il-´Ulamaa’

3 – al-Ijmaa´

Alikuwa na elimu iliopindukia katika kutambua tofauti za wanachuoni na dalili. Alikuwa ni Mujtahid asiyemfuata kipofu yeyote.

Shaykh Abu Ishaaq ash-Shiyraaziy alimtaja kuwa miongoni mwa wanachuoni wa Shaafi´iyyah.

Ametukhabarisha ´Umar bin ´Abdil-Mun´im: Ametukhabarisha al-Kindiy 608: Ametukhabarisha ´Aliy bin Hibatullaah: Ametukhabarisha Abu Ishaaq:

”Abu Bakr Muhammad bin Ibraahiym bin al-Mundhir an-Naysaabuuriy. Alikufa Makkah mwaka wa 309 au 310. Ametunga vitabu kuhusu tofauti za wanachuoni ambavyo havina mfano wake. Ambaye alikuwa akikubaliana naye na kwenda kinyume naye wote wawili walihitajia vitabu vyake. Sijui alichukua Fiqh kutoka kwa nani.”

Aliyotaja Abu Ishaaq kuhusu mwaka wake wa kufa si sahihi. Ibn ´Ammaar alikutana naye na akasikia kutoka kwake mwaka wa 316. Ibn-ul-Qattwaan al-Faasiy ameandika kwamba amefariki 318. Mwaka wa kwanza uliotajwa ni makosa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tadhkiyr-un-Naabihiyn, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 01/02/2019