01. Lengo la kutumwa Mitume na dalili juu ya hilo

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kwa Jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Jua – Allaah akurehemu – ya kwamba at-Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah (Subhaanah) kwa ´Ibaadah na ndio dini ya Mitume ambao Allaah aliwatuma kwayo kwa waja Wake. Wa kwanza wao ni Nuuh (´alayhis-Salaam). Allaah alimtuma kwa watu wake walipopetuka mipaka watu wema; Wadd, Suwaa´, Yaghuuth, Ya´uuq na Nasr.

Mtume wa mwisho ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na yeye ndiye alivunja picha za watu hawa wema. Allaah alimtuma kwa watu ambao wanaabudu, wanahiji, wanatoa swadaqah na wanamdhukuru Allaah kwa wingi, lakini waliwafanya baadhi ya viumbe kuwa, waasitwah, wakati kati baina yao na baina ya Allaah (Ta´ala). Wanasema: “Tunataka kutoka kwao sisi kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala) na tunataka uombezi wao Kwake; kama mfano wa Malaika, ´Iysa, Maryam na wengineo katika watu wema.

Allaah (Ta´ala) akawatumia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) awajadidie dini ya baba yao (´alayhis-Salaam) na kuwaeleza ya kwamba kujikurubisha huku na itikadi hii ni haki ya Allaah peke Yake, haisihi kufanyiwa katika hayo mwengine yeyote asiyekuwa Allaah, si Malaika aliyekaribu wala Mtume aliyetumwa, tusiseme wasiokuwa hao. Vinginevyo washirikina hawa walikuwa wakishuhudia ya kwamba Allaah ndiye Muumbaji pekee asiyekuwa na mshirika, na kwamba hakuna anayeruzuku isipokuwa Yeye, na hakuna anayehuisha wala kufisha isipokuwa Yeye, na wala hakuna anayeendesha mambo isipokuwa Yeye na kwamba mbingu zote saba na vilivyomo ndani yake, na ardhi saba na vilivyomo ndani yake, vyote hivyo [walikuwa wakiamini kuwa] ni viumbe Vyake na viko chini ya uendeshaji na Uwezo Wake.

Ukitaka dalili ya kwamba washirikina hawa ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapiga vita walikuwa wanashuhudia hili [yaani Tawhiyd-urRubuubiyyah], soma Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ

”Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini au nani anayemiliki kusikia na kuona na nani anayemtoa aliye hai kutoka mfu na anayemtoa mfu kutoka aliye hai na nani anayeendesha mambo?”  Watasema: “Ni Allaah”, basi sema: ”Je, basi kwa nini hamchi?”[1]

قُل لِّمَنِ الْأَرْضُ وَمَن فِيهَا إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ سَيَقُولُونَ لِلَّـهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ سَيَقُولُونَ لِلَّـهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ قُلْ مَن بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ سَيَقُولُونَ لِلَّـهِ ۚ قُلْ فَأَنَّىٰ تُسْحَرُونَ

”Sema: ”Ni ya nani ardhi na wale waliokuwemo humo mkiwa mnajua?” Watasema: ”Ni ya Allaah.” Sema: ”Je, basi hamkumbuki?” Sema: ”Nani Mola wa mbingu saba na Mola wa ‘Arshi kuu?” Watesema: ”Ni ya Allaah.” Sema: ”Je, basi kwa nini hamchi?” Sema: ”Nani katika mikono Yake uko ufalme wa kila kitu, Naye ndiye alindaye na wala hakilindwi chochote kinyume Naye, ikiwa mnajua?” Watasema: ”Ni Allaah pekee.” Sema: ”Basi vipi mnazugwa?”[2]

MAELEZO

Mwandishi (Rahimahu Allaah) amesema:

”Jua” – Akimlenga msomaji na muislamu ya kwamba Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah katika ´ibaadah. Hii ndio dini ya Allaah. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ

“Mungu wenu ni Mungu mmoja pekee; hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.”[3]

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ

“Mola wako ameamuru kwamba: “Msiabudu isipokuwa Yeye pekee.”[4]

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Wewe pekee ndiye tunakuabudu na Wewe pekee ndiye tunakuomba msaada.”[5]

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia yeye dini.”[6]

Tawhiyd ni kule kumpwekesha Allaah katika ´ibaadah. Ndio dini ya Mitume ambayo aliwatumiliza kwa waja Wake kuanzia wa mwanzo wao, ambaye ni Nuuh (´alayhis-Salaam), mpaka wa mwisho wao, ambaye ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

”Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut [waungu batili].”[7]

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.”[8]

Hapo kabla walikuwa juu ya dini ya Tawhiyd ambayo ni ya Nuuh na kabla yake Aadam (´alayhimaas-Salaam) na kizazi chake. Vivyo hivyo Mitume wengine baada yake walikuwa juu ya hili. Wakati kulipotokea shirki kwa watu wa Nuuh na wakashirikisha Wadd, Suwaa´, Yaghuuth na Nasr ndipo Allaah akawatumilizia Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili awakataze kuyaabudu mapicha na masanamu haya. Wao waliyatengeneza kwa lengo la kutaka kuwaiga. Walikuwa waja wema. Wakati walipofariki katika kipindi cha watu wa Nuuh ndipo shaytwaan  akawajia na akawaeleza sifa za waja hao na kwamba walikuwa waja wema na wabora. Akawashawishi watengeneza mapicha zao na waziweke katika vikao vyao ili waweze kuzikumbuka ´ibaadah zao na kuwaiga. Lengo lake mwishowe yawapelekee katika shirki au wale wataokuja baada yao. Wakatengeneza mapicha yao na wakayatundika katika vikao vyao mpaka kulipopita muda ndipo wakawaabudu badala ya Allaah. Wakati Allaah alipomtumiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawakaripia washirikina kuwaabudu waja wema na akawaeleza yale yaliyopitika kwa watu wa Nuuh. Kuliteremshwa juu ya tukio hilo Suurah “Nuuh”. Yeye ndiye ambaye alivunja mapicha ya waja hawa wema. Wadd, Suwaa´, Yaghuuth, Ya´uuq na Nasr walikuwa kwa waarabu. Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoukomboa mji wa Makkah akamwamrisha ayavunje.

[1] 10:31

[2] 23:84-89

[3] 02:163

[4] 17:23

[5] 01:05

[6] 98:05

[7] 16:36

[8] 21:25

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 07-09
  • Imechapishwa: 10/08/2020