Ulikuwa ukiniuliza juu ya imani na kutofautiana kwa watu juu ya kukamilika kwake, kuongezeka na kushuka kwake. Aidha unataka kujua yale waliyomo Ahl-us-Sunnah juu ya maudhui hayo na ni hoja zipi za wale wanaokwenda kinyume nao.

Hapo mwanzoni Salaf na wale waliowafuata mpaka hii leo wamezungumzia juu ya maudhui hayo. Nimekuandikia yale yote niyajuayo hali ya kumtakasia nia Allaah na kwa undani kabisa. Hata hivyo tambua kwamba wanachuoni na wale wenye kuitilia umuhimu dini wametofautiana kunako maoni mawili juu ya suala hilo:

1- Wamoja wamesema kuwa imani ni kule kumtakasia nia Allaah kwa moyo, kushuhudia kwa mdomo na matendo ya viungo.

2- Kundi jengine likasema kuwa imani ni kwa moyo na mdomo. Wanaona kuwa matendo  si jengine isipokuwa tu ni kumcha Allaah na wema na kwamba hayaingii katika imani.

Tukidurusu tofauti za hayo makundi mawili tunaona kuwa Qur-aan na Sunna vinasadikisha lile kundi la kwanza na kulirudi hilo kundi la pili.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 10
  • Imechapishwa: 25/02/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy