01. Kufunga Ramadhaan ni nguzo ya Uislamu


Himdi zote anastahiki Allaah. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Masahabah wake wote.

Amma ba´d:

Haya ni mambo madogo kuhusu swawm; hukumu yake, vigawanyo vyake, aina za watu,  vitu vinavyofunguza na faida nyenginezo kwa njia fupi.

1- Swawm ni kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala) kwa kujiepusha na vile vinavyofunguza tokea pale jua linapozama mpaka pale jua linapozama.

2- Kufunga Ramadhaan ni moja katika nguzo za Uislamu kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Uislamu umejengeka juu ya [mambo] matano; kushuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji nyumba tukufu.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nubadh fiys-Swiyaam, uk. 02
  • Imechapishwa: 15/05/2018