01. Kitabu cha ambaye anataka kuwafuata Salaf

Himdi zote anastahiki Allaah ambaye ni mtambuzi wa mambo yaliyofichikana na yenye kuonekana. Mipango na utashi Wake ni wenye kutekelezeka. Amepwekeka katika kuwaendesha viumbe na kuwarudisha. Anakadiria mwangamivu na mwenye furaha. Ameliumba kundi kwa ajili ya tofauti na ameliumba kundi kwa ajili ya ´ibaadah na akawafanya wawili hao kuwa katika makundi mawili; wale wenye kufanya vibaya na wale wenye kufanya mema bali na ziada. Swalah na salaam zimwendee mteuliwa bwana wetu Muhammad na kizazi chake.

Mimi nitataka kutaja madhehebu ya Salaf na wale waliowafuata kwa wema (Rahimahumu Allaah) katika majina na sifa za Allaah (Ta´ala), ili aweze kufuata njia yao yule atakayetaka kuwaiga na awe pamoja nao katika nyumba ya huko Aakhirah ikiwa atakuwa na ´Aqiydah yao. Yule mwenye kufuata na mwenye kufuatwa katika dunia hii watakuwa vilevile pamoja huko Aakhirah, katika kheri na shari. Amesema (Ta´ala):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

“Wale waliotangulia wa mwanzo [katika Uislamu] miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye.”[1]

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَيْءٍ

”Wale walioamini na wakafuatwa na dhuriya wao kwa imani, Tutawakutanisha nao dhuriya wao na hatutawapunguzia katika matendo yao kitu chochote.”[2]

 Amesema (Tabaarak wa Ta´ala) ya kwamba Ibraahiym (´alayhis-Salaam) amesema:

فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي

“Yule atakayenifuata, basi huyo ni katika mimi.”[3]

Vilevile amesema (Subhaanah):

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, Tutamgeuza alikogeukia na tutamuingiza Motoni – na ni uovu ulioje mahali pa kuishia!”[4]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

”Enyi walioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara marafiki wandani – wao kwa wao ni marafiki wandani – na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani, basi yeye ni katika wao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.”[5]

إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ ۖ وَبِئْسَ الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ

”Kwa Fir’awn na wakuu wake, lakini wakafuata amri ya Fir’awn na amri ya Fira’wn haikuwa yenye uongofu. [Fira’wn] atawatangulia watu wake siku ya Qiyaamah na atawafikisha Motoni – na ubaya ulioje mahali pa maingio watakapoingizwa!”[6]

 Kwa vile walimfuata hapa duniani, ndipo Akawafanya ni wenye kumfuata pia huko Aakhirah Motoni.

Imekuja katika khabari ya kwamba Allaah siku ya Qiyaamah atawaonyesha watu vile vyote walivyokuwa wakiviabudu, kama vile mawe, mti, jua na mwezi. Kisha awaambie:

“Huu si uadilifu Wangu kumfanya kila mmoja kufuata kile anachokuwa anaabudu duniani?” Kisha aseme: “Kila Ummah ufuate kila walichokiwa wanaabudu duniani.” Hivyo wavifuate mpaka viwatupe Motoni.”

Hali kadhalika kila yule anayemfuata kiongozi fulani hapa duniani, sawa iwe ni katika Sunnah, Bid´ah, kheri na shari, atakuwa naye huko Aakhirah. Kwa hiyo yule anayetaka kuwa pamoja na Salaf huko Aakhirah na aweze kuingia Peponi na yale waliyoahidiwa, basi awafuate kwa wema. Yule anayefuata njia isiyokuwa njia yao basi anaingia katika maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, Tutamgeuza alikogeukia na tutamuingiza Motoni – na ni uovu ulioje mahali pa kuishia!”

Kitabu hiki nimekifanya milango mitatu:

1- Mlango wa kwanza nazungumzia madhehebu yao.

2- Mlango unaosisitiza kuwafuata.

3- Mlango unaoweka wazi ya kwamba madhehebu yao ni ya sawa na haki.

Tunamuomba Allaah (Ta´ala) atuongoze sisi na waislamu wengine wote katika njia iliyonyooka na Atufanye sisi na wao kurithi neema za Peponi. Aamiyn.

[1] 09:100

[2] 52:21

[3] 14:36

[4] 04:115

[5] 05:51

[6] 11:97-98

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 6-8
  • Imechapishwa: 27/04/2018