01. Kila jambo muhimu linapaswa kuanzwa kwa jina la Allaah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

MAELEZO

Amekianza kitabu chake kwa:

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Hivo ndivo alivyokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye barua zake. Vilevile (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akianza mazungumzo yake pamoja na Maswahabah zake namna hiyo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kila jambo lenye umuhimu lisiloanzwa kwa jina la Allaah ni lenye kukosa baraka.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Kila jambo lenye umuhimu lisiloanzwa kwa shukurani zote njema anastahiki Allaah… “

Mambo yote muhimu (kama mfano wa vitabu, khutbah, mihadhara, kula na kunywa) mtu anatakiwa aanze kwa jina la Allaah ili vibarikiwe. Baadhi ya watu hawaanzi kwa jina la Allaah mwanzoni mwa vitabu vyao. Hivyo wanakuwa ni mwenye kwenda kinyume na Sunnah na wamewagiliza wamagharibi. Vinginevyo kila muislamu anapaswa kuanza kwa jina la Allaah kwenye vitabu vyake, khtubah zao, mihadhara yao na barua zao. Mashairi yenye uchokozi na yenye semwa vibaya hatakiwi kuanzwa kwa jina la Allaah. Wala maneno yenye matusi na maneno mabaya. Mashairi mazuri yaanzwe kwa jina la Allaah. Kwa ajili hiyo ndio maana kila Suurah ndani ya Qur-aan tukufu imeanzwa kwa jina la Allaah isipokuwa tu at-Tawbah. Wanachuoni wamesema kwamba ni kwa sababu al-Anfaal na at-Tawbah zote mbili zinazungumzia mambo ya vita. Zinazungumzia mada moja na ni kama kwamba ni Suurah moja. Suurah zengine zote zinaanzwa kwa jina la Allaah kama tulivyotangulia kusema. Wanachuoni wanasema kuwa maana yake ni mtu anaomba msaada au anaanza barua yake, kitabu chake au maneno yake kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

[1] Haafidhw as-Suyuutwiy (Rahimahu Allaah) ameinasibisha katika ”al-Arba´uun” ya ´Abdul-Qaadir ar-Raahaawiy kisha akaeleza kuwa ni dhaifu. (al-Jaami´ as-Swaghiyr, uk. 391)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 06/08/2019