01. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah

Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amma ba´d: Hii ni I´tiqaad ya al-Firqat-un-Naajiyah al-Mansuurah mpaka kisimame Qiyaamah, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, nayo ni:

MAELEZO

Amma ba´d – Hili ni neno ambalo huletwa pindi mtu anapotaka kutoka katika usulubu mmoja kwenda katika usulubu mwengine. Maana yake ni vile itakavyokuwa. Imependekezwa kuleta neno hili katika Khutbah na wakati wa kuandika kwa ajili ya kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu alikuwa akifanya hivo.

Hii – Ni ishara ya zile I´tiqaad za kiimani zilizomo ndani ya kitabu hiki ambazo amezikusanya kwa kusema:

“Nayo ni kumuamini Allaah… “

´Aqiydah – Ni kile ambacho anakiimanisha mtu ndani ya moyo wake. Husemwa “Niliitakidi hivi” bi maana moyo umefungamanishwa nacho. Msingi wake imechukuliwa kutoka katika kifungo cha kamba pindi inapofungwa. Halafu ikatumiwa katika I´tiqaad ya moyo.

al-Firqah – Pote na kundi.

an-Naajiyah – Bi maana ambalo limesalimika kutokamana na maangamivu na shari duniani na Aakhirah na likafikira uokovu na furaha. Sifa hii imechukuliwa kutoka katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Halitoacha kundi kutoka katika Ummah wangu kuwa juu ya haki hali ya kuwa ni lenye kunusuriwa. Halitodhurika na wale wenye kulikosesha nusura mpaka ifike amri ya Allaah.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

al-Mansuurah – Bi maana lenye kutiwa nguvu juu ya wale wenye kwenda kinyume nalo.

Mpaka kisimame Qiyaamah – Kufika Qiyaamah ni kule kufa kwao pindi utapokuja upepo ambao utamuua kila muumini. Hiki ndio Qiyaamah juu ya waumini.

Kuhusu Qiyaamah ambacho kina maana kwamba kuisha kwa dunia hakitowasimamia isipokuwa kwa watu waovu. Hayo yamepokelewa na Muslim katika “as-Swahiyh” yake:

“Hakitosimama Qiyaamah isipokuwa hakutokuwa ardhini yeyote ambaye anasema “Allaah! Allaah!”

Ameipokea Imaam al-Haakim kupitia Hadiyth ya ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Ndani yake imekuja:

“Allaah atatuma upepo wenye harufu kama miski ambao utagusa kama inavyogusa hariri. Haitoacha nafsi yoyote ambayo ndani yake kuna chembe kidogo ya imani isipokuwa itamchukua. Kisha kutabaki watu waovu. Hao ndio watasimamiwa na Qiyaamah.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 02-06
  • Imechapishwa: 07/02/2018