Mfumo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun wanaharakati wana sifa zinazokataliwa na kila mwanafunzi anayetambua hadhi ya elimu na kutenda kazi kwa mujibu wake, kumcha Allaah na kuchunga haki Zake na haki za waja Wake. Tutazitaja baadhi yake ili yule aliyedanganywa anufaike nazo na kurudi katika akili yake timamu na ili vilevile kuwanufaisha watu werevu na khaswa vijana wanaopenda kheri na kulingania katika dini ya Allaah:

1- Wanatilia umuhimu mkubwa kuwaingiza vijana katika fikira za al-Ikhwaan al-Muslimuun zilizotolewa nje ya nchi hii. Aliyeiasisi ni Hasan al-Bannaa (aliyefariki. 1347). Wao hawatazami yule anayejinasibisha na mfumo wao ni Suuniy, mzushi hata kama atakuwa ni Raafidhwiy. Hili linathibitisha kuwa hawana yale mapenzi na chuki iliyowekwa katika Shari´ah kwa ajili ya Allaah. Allaah awaongoze!

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 25/03/2017