01. Hadiyth “Yule mwenye kuulizwa juu ya elimu… “

120- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuulizwa juu ya elimu akaificha, basi atapigwa hatamu ya Moto siku ya Qiyaamah.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy aliyesema kuwa ni nzuri, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh”, al-Bayhaqiy na al-Haakim amepokea mfano wake na akasema:

“Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Lakini hawakuitoa.”

Katika upokezi wa Ibn Maajah imekuja:

“Hakuna mtu yeyote atakayehifadhi elimu kisha akaificha isipokuwa atalaletwa siku ya Qiyaamah amepigwa kwa hatamu ya Moto.”[2]

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/160)
  • Imechapishwa: 03/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy