01. Hadiyth “Yule atakayesimama usiku wa makadirio kwa imani na kwa matarajio… “


992- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesimama usiku wa makadirio kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia. Yule atakayefunga Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah kwa mukhtaswari. Katika upokezi wa an-Nasaa´iy imekuja ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayefunga Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia. Yule atakayesimama usiku wa makadirio kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia.”[2]

al-Khattwaabiy amesema:

“Imani na kwa matarajio bi maana kwa nia na kwa maazimio. Anatakiwa kufunga kwa kusadikisha na kwa kutarajia thawabu zake, kwa furaha na si kwa kutokutaka. Hatakiwi kuona kuwa ni kero au kuona kuwa michana ni mirefu. Lakini badala yake anatakiwa kutumia fursa ya michana mirefu juu ya lukuki ya thawabu.”

al-Baghawiy amesema:

“Kwa matarajio hali ya kuwa ni mwenye kutafuta uso wa Allaah (Ta´ala) na thawabu Zake.”

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/582)
  • Imechapishwa: 12/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy