01. Hadiyth “Yule ambaye Allaah anamtakia kheri… “

67- Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri basi humfanya akaielewa dini.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Maajah. at-Twabaraaniy pia ameipokea katika “al-Kabiyr” kwa muundo usemao: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Enyi watu! Hakika elimu [hufikiwa] kwa kujifunza na uelewa [hufikiwa] kwa kuelewa. Yule ambaye Allaah anamtakia kheri basi humfanya akaielewa dini na:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni.”[2][3]

Katika cheni ya wapokezi kuna mpokezi asiyetambulika[4].

[1] Swahiyh.

[2] 35:28

[3] Nzuri kupitia zengine.

[4] Ina njia zengine na mapokezi yanayoitolea ushahidi yanayotilia nguvu. Tazama ”as-Swahiyhah” (342).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/136)
  • Imechapishwa: 02/09/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy