37- al-´Irbaadhw bin Saariyah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituwaidhi mawaidha ambayo nyoyo ziliingiwa na khofu kwayo na macho yakatokwa na machozi. Tukasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni kana kwamba ni mawaidha ya kutuaga, hivyo basi tuusie.” Akasema: “Nakuusieni kumcha Allaah, na kusikiliza na kutii hata kama atatawalia juu yenu mja. Hakika yule atakayeishi muda mrefu katika nyinyi basi atakuja kuona tofauti nyingi. Hivyo basi, lazimianeni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu. Ziumeni kwa magego yenu. Ninakutahadharisheni na mambo yaliyozuliwa, kwani hakika kila Bid´ah ni upotevu.”

Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiiyh”. at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) “Ziumeni kwa magego yenu” maana yake ni kwamba jitahidini kuwa juu ya Sunnah, lazimianeni nazo na zipupieni, kama ambavo mtu anang´ata kitu kwa magego yake kwa kuchele kisije kuondoka na kumponyoka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/453)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy