1063- Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuleni daku[1]. Kwani hakika katika daku kuna baraka.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.

[1] Wanachuoni wameafikiana kwamba daku imependekezwa na sio lazima. Kitendo cha daku kuwa na baraka ni jambo liko wazi. Kwa sababu inampa mtu nguvu na uchangamfu wa kufunga na matokeo yake kumfanya mtu kuendelea kuwa na morali ya kufunga kwa sababu ya wepesi wa ugumu. Zipo maana na tafsiri zengine zilizotolewa na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/619)
  • Imechapishwa: 22/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy