1053- Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mwaka ulipofunguliwa mji wa Makkah Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kuelekea Makkah katika Ramadhaan. Watu walikuwa wamefunga. Mpaka alipofika Kuraa´-ul-Ghamiym akaomba chombo cha maji. Akakinyanyua ili watu wapate kumuona kisha akakinywa. Baada ya hapo akaambiwa kuwa kuna watu waliofunga ambapo akasema: “Hao ni waasi. Hao ni waasi.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Akaambiwa: “Baadhi ya watu swawm imekuwa ngumu kwao na wanasubiri waone utachofanya.” Ndipo akaomba chombo cha maji baada ya ´Aswr.”

Ameipokea Muslim.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/587)
  • Imechapishwa: 21/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy