01. Hadiyth “Hakika miongoni mwa matendo na mema yanayomwandama muumini… “

112- Abu Hurayrah amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika miongoni mwa matendo na mema yanayomwandama muumini baada ya kufa kwake ni elimu aliyofunza na aliyoeneza, mtoto mwema aliyemwacha nyuma, Mushafu aliyoacha anarithisha, msikiti aliyojenga, nyumba kwa ajili ya wapitanjia aliyojenga, kisima alichochimba au swadaqah kutoka katika mali yake aliyoitoa wakati akiwa na afya njema na bado akiwa hai – mambo haya yanaandamana naye baada ya kufa kwake.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi nzuri, al-Bayhaqiy na Ibn Khuzaymah amepokea mfano wake katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/156)
  • Imechapishwa: 03/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy