01. Hadiyth “Allaah ampambe mtu ambaye amesikia kitu kutoka kwetu… “

89- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Allaah ampambe mtu ambaye amesikia kitu kutoka kwetu ambapo akakifikisha kama alivokisikia. Huenda mfikishaji ana uelewa mzuri zaidi kuliko msikilizaji.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud[2], at-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” kwa tamko lisemalo:

“Allaah amrehemu mtu… “

at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Abu Daawuud hakuipokea kutoka kwa Ibn Mas´uud, bali ameipokea kutoka kwa Zayd bin Thaabit inayokuja baada ya hii.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/147)
  • Imechapishwa: 01/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy