01. Dalili juu ya mguu wa Allaah


1- Haramiy bin ´Umrah ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Qataadahh, kutoka kwa Anas aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kutatupwa Motoni na useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Hakuna zaidi?”[1]

mpaka Mola wa walimwengu aweke mguu Wake – au unyayo Wake – ndani yake ambapo utasema: “Tosha, tosha.”[2]

[1] 50:30

[2] al-Bukhaariy (4848), Muslim (2188), Ahmad (3/129), at-Tirmidhiy (3272), an-Nasaa’iy katika ”al-Kubraa” (7719), ad-Daarimiy katika ”ar-Radd ´alaa Bishr al-Mariysiy, uk. 69, al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 348-349, Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 92-93, na Ibn Mandah katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 42, ambaye amesema:

”Hadiyth imethibiti kwa maafikiano.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 18/10/2017