00. Utangulizi wa “Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal”


Himdi zote anastahiki Allaah. Tunamhimidi yeye, tunamuomba msaada, msamaha na tunatubia Kwake. Tunajilinda kwa Allaah kutokamana na shari ya nafsi zote na uovu wa matendo yetu. Yule aliyeongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpotosha, na yule aliyepotoshwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa ni Mmoja pekee asiyekuwa na mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Allaah amemtumiliza karibu na kusimama Qiyaamah hali ya kuwa ni mwenye kutoa bishara njema na mwenye kuonya na mwenye kulingania kwa Allaah kwa idhini Yake na taa lenye kuangaza. Akafikisha ujumbe, akatekeleza amana, akautakia mema Ummah na akapambana katika njia ya Allaah ipasavyo – swalah na salamu ziwe juu yake, kizazi chake, Maswahabah zake na wale watakaomfuata kwa wema hadi siku ya Qiyaamah. Allaah (Ta´ala) amesema:

Amma ba´d:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja na Akaumba kutoka humo mke wake na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana na jamaa. Hakika Allaah Amekuwa juu yenu ni Mwenye kuchunga.”[1]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا

“Enyi mlaomini! Mcheni Allaah na semeni kauli ya kweli [ya sawasawa]. Atakutengenezeeni ‘amali zenu na Kukusameheeni madhambi yenu; na anayemtii Allaah na Mtume Wake, basi kwa yakini amefanikiwa mafaniko adhimu.”[2]

[1] 04:01

[2] 33:70-71

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 05-06
  • Imechapishwa: 18/06/2019