00. Utangulizi wa “Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah”

Himdi zote anastahiki Allaah. Tunamhimidi Yeye, kumtaka msaada na msamaha. Tunajilinda Kwake kutokamana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yule aliyehidiwa na Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na yule aliyepotezwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.

Amma ba´d:

Utashi umepelekea katika kuwasahilishia elimu watu wote katika kuzikunjua ´ibaadah za hijah. Nimefanya hivo kwa kufupisha kitabu changu “Hajjat-un-Nabiyy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamaa rawaahaa ´anhu Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh)”. Nimefanya hivo kama ule mtindo niliofanya katika kitabu changu “Takhiysw Swifah Swalaat-in-Nabiyy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)”. Isipokuwa tu humu ndani nimeongeza nyongeza muhimu na nimesawazisha baadhi ya pengu za ´ibaada za hajj ambazo hazikutajwa katika “Hajjat-un-Nabiyy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)” au maelezo yake.

Nimepatiliza upatilizo maalum katika kuzitaja nyongeza hizi na kadhalika faida zengine, kwa ule mfumo wangu wa kawaida, kama vitabu vyengine vyote. Kama mfano wa daraja za Hadiyth na marejeo yake. Hata hivyo nimefanya hivo kwa njia ya kufupiza pamoja na kuashiria kukupeleka katika vitabu vyengine baadhi ya nyakati ambavyo vimeshachapishwa na ambavyo bado havijachapishwa.

Kuhusu yale ambayo tayari yaliyomo katika “Hajjat-un-Nabiyy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)”, sikutaja marejeo ya Hadityh. Kwa sababu ya kutoshelezeka kwa kuenea kwa kitabu kwa wasomaji watukufu. Kwa hivyo yule anayetaka kuhakikisha kitu huko, basi rahisi arejee huko. Pindi ninapokinakili basi huashiria kwa neno “msingi”.

Kwa ajili ya kutimiza faida zaidi, nimetaja baadhi ya mambo kwa ufupi na kuyaweka katika Bid´ah za hajj na kutembelea msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kitabu nimekipa jina “Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah fiyl-Kitaab was-Sunnah wa Aathaar -is-Salaf”.

Ninamuomba Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) akifanye kitendo changu chote kiwe chema na akifanye kiwe kwa ajili Yake pekee na si kwa mwengine.

21 Sha´baan 1395

Dameski

Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 5-6
  • Imechapishwa: 12/08/2017