00. Utangulizi wa “al-Wasaa-il-ul-Mufiydah”

Himdi ni Zake Allaah ambaye ndiye ana himdi zote njema. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa pekee hana mshirika na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake – swalah na salamu zimwendee yeye, kizazi chake na Maswahabah zake.

Amma ba´d:

Hakika raha na furaha ya moyo na kuondoka kwa misononeko na msongo wa mawazo ndio lengo la kila mmoja. Kupitia hayo ndio kunapatikana maisha mazuri na kukatimia furaha na tabasamu. Kwa hayo zipo sababu za dini, za kimaumbile na za kimatendo. Mambo haya yote hayawezi kumkusanyikia isipokuwa muumini peke yake. Kuhusu wengineo – ingawa wanaweza kupata sehemu katika hayo ambayo wale wenye busara katika wao wanayaendea mbio kwelikweli – basi yatawapita kwa njia ambazo ni zenye manufaa, imara, nzuri zaidi na za matokeo mazuri zaidi.

Lakini katika kijitabu hichi nitataja zile sababu ninazokumbuka juu ya lengo hili kuu ambalo ndio analiendea mbio kila mmoja.

Miongoni mwa watu wako ambao wamepata sehemu yake kubwa na hivyo wakaishi maisha yenye utulivu na mazuri.

Miongoni mwa watu wako  ambao wamezikosa zote na hivyo wakaishi maisha ya tabu na mabaya zaidi.

Miongoni mwa watu wako  ambao wameishi baina ya hayo mawili kwa kiasi cha vile walivyojaaliwa.

Allaah ndiye mwenye kuongoza na mwenye kutakwa msaada juu ya kila kheri na juu ya kuzuia kila shari.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 03/05/2020