00. Uislamu wa jadi ni Uislamu wa Salaf


Shaykh Abu ´Aliy al-Hasan bin ´Umar bin Abiy Bakr bin Zakariyyaa ametukhabarisha: Shaykh na Imaam Muhammad bin al-Husayn bin al-Qaasim as-Suufiy at-Tikriytiy ametuhadithia kupitia riwaya yake kutoka kwa Imaam Jamaal-ud-Diyn Abu Ja´far Ahmad bin Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz al-Makkiy Abul-Wafaa: Shaykh, Imaam na Faqiyh Abul-Qaasim Sa´d bin ´Aliy bin Muhammad az-Zinjaaniy (Radhiya Allaahu ´anh) ametukhabarisha:

Himdi zote njema anastahiki Allaah kwa hali zote. Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad mteule na wale Maswahabah na kizazi wazuri.

Umeniuliza juu ya ´Aqiydah ya Salaf na wale wema waliokuja nyuma juu ya sifa za Allaah zilizothibiti ndani ya Qur-aan na Sunnah Swahiyh na umetaka nijibu kwa kifupi. Hivyo nikamtaka Allaah (Ta´ala) ushauri na nikajibu kwa jawabu alilojibu mwanachuon, naye si mwengine ni Abul-´Abbaas Ahmad bin ´Umar bin Surayj. Kwani yeye pia aliulizwa swali kama hilo. Faqiyh Abu Sa´d ´Abdul-Waahid bin Muhammad amesema: Nimesikia kikosi cha wanazuoni wenye kushikamana na mapokezi na mfumo wa kizazi cha kwanza wakisema: Ibn Surayj aliulizwa kuhusu sifa za Allaah na upwekekaji Wake ambapo akasema yafuatayo…

  • Mhusika: Imaam Abul-Qaasim Sa´d bin ´Aliy bin Muhammad az-Zinjaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ajwibah fiy Usuul-id-Diyn, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 10/06/2021