00. Dibaji ya kitabu al-Mu´taqad as-Swahiyh

Himdi zote ni stahiki ya Allaah. Swalah na salamu ziwe juu ya Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Amma ba´d:

Hakika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ndio dini ya haki ambayo ni wajibu kwa kila muislamu aiitakidi, kwani ndio ´Aqiydah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake watukufu (Radhiya Allaahu ´anhum). Atakayechagua ´Aqiydah nyingine, basi ameipelekea nafsi yake katika adhabu, hasira na ghadhabu za Allaah kali.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu mapote ambayo yatazuka katika Ummah wake na akataja mapote sabini na tatu:

“Yote yatakuwa Motoni isipokuwa moja tu ambalo ni al-Jamaa´ah.”[1]

Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesifu mkusanyiko huu ambao umesalimika kutokamana na matishio ya Moto pale aliposema:

“Ni wale wataokuwemo katika mfano wa yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”[2]

Hiki ndio kidhibiti na kigezo cha Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hakika wao ni wenye kushikamana barabara na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Sunnah za makhaliyfah wake waongofu. Ni wenye kuziuma kwa magego. Kwa ajili hio ndio maana wakawa ni pote lililookoka (Firqat-un-Naajiyah). Ni wenye kuokoka na Moto siku ya Qiyaamah. Ni wenye kusalimika na Bid´ah hapa duniani. Vilevile wao ni kundi lililonusuriwa (Firqat-ul-Mansuurah). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakutoacha kuwepo kipote katika Ummah wangu kuwa ni chenye kushinda mpaka itapowajia amri ya Allaah ilihali ni wenye kushinda.”[3]

Maana ya ushindi hapa (الظُّهور) ni nusura. Amesema (Ta´ala):

فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ

“Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi.” (61:149)

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ

“Na hakika jeshi Letu ndilo litakaloshinda.” (37:173)

Wao ni wenye kushinda kwa panga na mikuki au kwa hoja na dalili.

Inahusu kundi moja na sio mengi. Kwa ajili hiyo ndio maana wameitwa ´mkusanyiko`. Amesema (Ta´ala):

فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ

“Na kuna nini baada ya haki isipokuwa upotofu?” (10:32)

Hawatambuliki kwa jina jengine zaidi ya Uislamu na Sunnah na yale matamshi yaliyofahamishwa na hayo mawili. Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ahl-us-Sunnah hawana jina jengine wanalotambulika kwalo, si Jahmiyyah, Qadariyyah wala Raafidhwah.”

Aliulizwa vilevile kuhusu as-Sunnah ambapo akajibu kwa kusema:

“Hawana jina jengine zaidi ya as-Sunnah.”

Bi maana Ahl-us-Sunnah hawana jina wanalojinasibisha nalo zaidi ya hilo.

Kumetiliwa umuhimu mkubwa juu ya kuipa nguvu ´Aqiydah ya wema waliotangulia (Salaf-us-Swaalih) na kubainishwa dalili zake. Imewekwa wazi na maimamu wengi wakubwa katika vitabu vingi, vya kujitegemea na vya kwa pamoja. Miongoni mwa vitabu hivyo kuna vinavyoitwa “as-Sunnah”, bi maana “´Aqiydah”. Ni zaidi ya vitabu mia mbili na khamsini. Baadhi yavyo ni:

1- ”as-Sunnah” ya Ibn Abiy Shaybah

2- “as-Sunnah” ya Ahmad bin Hanbal

3- ”as-Sunnah” ya Ibn Abiy ´Aaswim

4- ”as-Sunnah” ya ´Abdullaah bin Ahmad

5- ”as-Sunnah” ya al-Khallaal

6- ”as-Sunnah” ya Ahmad bin al-Furaat Abiy Mas´uud ar-Raaziy

7- “as-Sunnah” ya al-Asad bin Muusa

8- ”as-Sunnah” ya Ibn-ul-Qaasim – mwanafunzi wa Maalik

9- ”as-Sunnah” ya Muhammad bin Salaam al-Baykandiy.

10- “as-Swiffaat wa ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah” ya Abu Nu´aym bin Hammaad

11- ”as-Sunnah” ya al-Athram

12- ”as-Sunnah” ya Harb bin Ismaa´iyl al-Karmaaniy

13- ”as-Sunnah” ya Ibn Abiy Haatim

14- ”as-Sunnah” ya Ibn Abiyd-Dunyaa

15- ”as-Sunnah” ya Ibn Jariyr at-Twabariy.

16- “at-Tabswiyr fiy ma´aalim-in-Diyn” na huyohuyo Ibn Jariyr pia

17- ”as-Sunnah” ya at-Twabaraaniy

18- ”as-Sunnah” ya Abush-Shaykh al-Aswbahaaniy

19- ”as-Sunnah” ya Abul-Qaasim al-Laalakaa’iy

20- ”as-Sunnah” ya Muhammad bin Naswr al-Marwaziy

21- ”´Aqiydat-us-Salaf wa Asw-haab-il-Hadiyth” ya as-Swaabuuniy

22- ”al-Ibaanah” ya Ibn Battwah

23- ”at–Tawhiyd” ya Ibn Khuzaymah

24- ”at-Tawhiyd” ya Ibn Manda

25- ”al-Iymaan” ya Ibn Abiy Shaybah

26- ”al-Iymaan” ya Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam

27- ”Sharh-us-Sunnah” ya al-Muzaniy – mwanafunzi wa ash-Shaafi´iy

28- ”Sharh Madhaahib Ahl-is-Sunnah” ya Ibn Shaahiyn

29- ”al-Hujjah fiy Bayaan-il-Mahajjah wa Sharh ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah” ya Abul-Qaasim al-Aswbahaaniy

30- ”Usuul-us-Sunnah” ya Abu Abdullaah Ibn Abiy Zamaniyn

31- ”ash-Shariy´ah” ya al-Aajurriy

32- ”I´tiqaad Ahl-is-Sunnah” ya Abu Bakr al-Ismaa´iyliy

33- ”as-Sunnah” ya al-Barbahaariy

34- ”al-Iymaan” ya Ibn Manda

35- ”al-Iymaan” ya al-´Adaniy

36- ”al-´Arsh” ya Ibn Abiy Shaybah

37- ”al-Qadar” ya Ibn Wahb

38- ”al-Qadar” ya Abu Daawuud

39- ”ar-Ru’yah” ya ad-Daaraqutwniy

40- ”as-Swifaat” ya ad-Daaraqutwniy

41- ”an-Nuzuul” ya ad-Daaraqutwniy

42- “Risaalat-us-Sijziy ilaa Ahl-iz-Zabiyd” Abu Naswr as-Sijziy

43- ”Jawaab Ahl Dimashq fiys-Swifaat” ya al-Khatwiyb al-Baghdaadiy

44- “as-Sunnah” ya Abu Ahmad al-Aswbahaaniy kwa jina maarufu al-´Assaal

45- “as-Sunnah” ya Ya´quub al-Fasawiy

46- “as-Sunnah” ya al-Qasswaab

47- “Usuwl-us-Sunnah” ya Abu Bakr bin ´Abdillaah bin az-Zubayr al-Humaydiy

48- “as-Sunnah” ya Hanbal bin Ishaaq

49- “al-Usuwl” ya Abu ´Amr at-Twalamankiy

na vitabu vinginevyo vingi.

Vivyo hivyo inahusiana na vitabu vilivyoandikwa baada ya waandishi hawa. Miongoni mwao ni Ibn ´Abdil-Barr, ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy, Ibn Qudaamah al-Maqdisiy, Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim, adh-Dhahabiy, Ibn Kathiyr, Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na wengineo. Humo mmebainishwa ´Aqiydah sahihi. Vinasimamisha hoja na kufichua hoja tata za Ahl-ul-Ahwaa´.

Tutataja sehemu katika ´Aqiydah ya watu hawa vigogo kwa njia ya kufupiza.

Sipati kuwezeshwa haya isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Kwake Yeye ninategemea na kwake Yeye narejea.

[1] Ahmad na Abu Daawuud kutoka kwa Mu´aawiyah na ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim, adh-Dhahabiy, ash-Shaatwibiy na wengineo. Ahmad, Ibn Maajah na Ibn Abiy ´Aaswim kutoka kwa Anas.

[2] Ameipokea al-Aajurriy katika “ash-Shariy´ah” kutoka ´Abdullaah bin ´Amr na at-Twabaraaniy katika “as-Swaghiyrah” na katika “al-Awsatw” kutoka kwa Anas bin Maalik.

[3] Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa al-Mughiyrah bin Shu´bah.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mu´taqad as-Swahiyh, uk. 5-11
  • Imechapishwa: 20/06/2020