00. Utangulizi wa “Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´”

Himdi zote zinamstahikia Allaah. Tunamhimidi Yeye, kumtaka msaada na msamaha. Tunajilinda Kwake kutokamana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yule mwenye kuongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na yule mwenye kupotezwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa pekee hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na ni Mtume wake. Allaah (Ta´ala) amemtuma kwa uongofu na dini ya haki ambapo akawa ni mwenye kufikisha ujumbe, akatekeleza amana, akaupendea kheri Ummah na akapambana kwa ajili ya Allaah ukweli wa kupambana – swalah na salaam ziwe juu yake yeye, kizazi chake, Maswahabah wake na wale wote watakaowafuata kwa wema mpaka siku hiyo ya mwisho.

Amma ba´d:

Nafurahi kuhudhuria chuo kikuu cha sekondari cha wasichana Jeddah siku hii ya leo jumanne 23 Rabiy´ ath-Thaaniy mwaka 1412 ili kuzungumzia yale yaliyomo ndani ya nafsi yangu juu ya mada hii muhimu ”Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´”. Nasema hali ya kuwa ni mwenye kumtaka msaada Allaah (´Azza wa Jall) na nikimuomba mafanikio na uimara:

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017