0. Dibaji ya “Hukm Taarik-is-Swalaah”

Himdi zote anastahiki Allaah. Tunamhimidi Yeye na kumuomba msaada na msamaha. Tunajilinda Kwake kutokamana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Aliyeongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na aliyepotezwa na Allaah, hakuna wa kumwongoza. Ninashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa ni Mmoja hana mshirika. Ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Swalah na salaam ziwe juu yake yeye, kizazi chake na Maswahabah zake mpaka siku ya Qiyaamah.

Amma ba´d:

Hakika waislamu wengi leo wameichukulia sahali na kuipuuza swalah kiasi cha kwamba mpaka baadhi yao wamefikia kuiacha kabisa kabisa kwa sababu ya uvivu. Mada hii ilipokuwa ni kubwa ambayo watu wa leo wamepewa mtihani kwayo na wakatofautiana kwayo wanachuoni katika zama zote, nikapendelea kuandika kuhusiana na mada hiyo kile kitachowezekana. Kijitabu kitagusia maudhui mbili:

1- Hukumu ya mwenye kuacha swalah.

2- Yanayopelekea kwa kuritadi kwa sababu ya kuacha swalah na nyenginezo.

Ninamuomba Allaah (Ta´ala) aniwafikishe katika usawa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 2
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 22/10/2016