00. Dibaji “al-Ibdaa´ fiy Kamaal-ish-Shar´ wa Khatwar-il-Ibtidaa´”

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

Himdi zote njema anastahiki Allaah. Tunamuhimidi Yeye na kumuomba msaada na msamaha. Tunajilinda Kwake kutokana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yule ambaye ameongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpotosha, na yule ambaye amepotoshwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirikina, na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mtumwa na Mtume Wake. Allaah (Ta´ala) alimtuma kwa uongofu na dini ya haki. Akafikisha Ujumbe, akatekeleza amana, akaunasihi Ummah na akapambana kwa ajili ya Allaah ukweli wa kupambana mpaka alipofariki. Akauacha Ummah wake katika njia nyeupe kabisa; usiku wake ni kama mchana wake na hakuna atayepinda nayo isipokuwa mwangamivu. Amebainisha humo yale Ummah  wanayahitaji. Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumwacha ndege anayepiga kwa mbawa zake mbinguni isipokuwa ametufunza kitu juu yake.”[1]

Kuna mshirikina mmoja alimwambia Salmaan al-Faariysiy (Radhiya Allaahu ´anh):

”Mtume wenu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekufunzeni mpaka adabu za kukidhi haja.” Salmaan akasema: ”Ni kweli. Ametukataza kuelekea Qiblah wakati wa kukidhi haja ndogo na kubwa na kutamba kwa mawe chini ya matatu, kutamba kwa mkono wa kulia na kutamba kwa kinyesi na mifupa.”[2]

[1] Ahmad (21689), (2188) na (21771).

[2] Muslim (262).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibdaa´ fiy Kamaal-ish-Shar´ wa Khatwar-il-Ibtidaa´, uk. 2
  • Imechapishwa: 23/10/2016