Mzee ambaye kishatokwa na akilini amekufa akiwa na deni la Ramadhaan

Swali: Mama yangu ana miaka kati ya 85-90 ambaye amepatwa na maradhi ya shinikizo la damu, kisukari na maradhi ya moyo. Haya ni kwa mujibu wa uthibitisho wa daktari. Ameshapitiwa na kipindi kirefu ambacho baadhi yake alilazwa hospitalini na baadhi yake nyumbani mpaka akafariki. Haya pamoja na kuzingatia ya kwamba wakati mwingine anapoteza fahamu na anauliza maswali mengi ya kukariri na anawaomba wafu kwa muda mrefu. Mfano wa anaowaomba ni ndugu zake. Mimi sijui haya yanatokamana na maradhi au ni kwa sababu ya utuuzima. Nukta niliyokuwa nataka kulenga ni kwamba Ramadhaan ya mwaka 1409 ilimpitikia mama yangu akiwa katika hali hii niliyowaeleza. Ni wajibu kumfungia? Ikiwa ni wajibu kumfungia afungiwe na mmoja katika watoto zake au kila mmoja anaweza kumfungia baadhi ya siku au ni wajibu kumtolea swadaqah? Ikiwa ni wajibu kumtolea swadaqah ni lipi ambalo ni bora; kumtolea swadaqah katika mali zake yeye binafsi au katika mali za watoto wake haya kwa kuzingatia ya kwamba ana watoto wengi wa kiume na wa kike? Ikiwa ni wajibu kumtolea swadaqah ni kiwango gani kwa kila siku moja ya Ramadhaan? Ni aina ya vitu gani na ni kunatumiwa njia gani katika utoaji?

Jibu: Mambo yakiwa kama alivyosema muulizaji hakuna kinachomlazimu kutokana na kasoro iliyomo akilini mwake. Kutokana na hayo inapata kujulikana ya kwamba haikulazimuni kumfungia wala kumtolea fidia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/167-168)
  • Imechapishwa: 04/06/2017